The House of Favourite Newspapers

Kisa Kukosoa Maandiko ya Biblia, Nabii Amtaka Nikki Wa Pili Atubu – Video

Nabii wa Kanisa la Ufukufu kwa Bwana amemtaka Rapa maarufu nchini, Nikki Wa Pili kutubu kutokana na kauli yake aliyoandika kwenye akaunti yake ya Twitter hivi karibuni juu ya uumbaji wa Mungu kwa kusema kuwa huenda binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni mwanamke badala ya mwanamme kama maandiko yanavyosema.

 

Nikki alisema kuwa maneno ya kwenye biblia yanayosema binadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu alikuwa ni mwanamme yanatokana na hali ilivyokuwa kwa wakati ule, na yalikuwa ni ya kimfumo dume.

MSIKIE NABII AKIFUNGUKA

Comments are closed.