The House of Favourite Newspapers

Kisa Magufuli, Diamond, Harmonize Waingia Studio -Video

0

KUFUATIA kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kilichotokea juzi Jumatano, wasanii mbalimbali waliingia studio na kurekodi nyimbo kwa ajili ya kumuenzi kiongozi huyo.

Msanii Harmonize akiwa na wenzake wa Konde Gang waliingia studio na kutoa wimbo walioupa jina la Asante Magufuli ukielezea namna Magufuli alivyoacha alama kwa mazuri aliyoyafanya Wakati huohuo, wasanii wengine wakiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny, Jux, Marioo, Malkia Karen, Zuchu, Khadija Kopa, Christina Shusho, Gnako, Abbah na S2kyz walikutana katika studio za Wanene kwa ajili ya kurekodi kazi za kumuenzi Magufuli.

STORI: JOHN JOSEPH, DAR ES SALAAM

Leave A Reply