The House of Favourite Newspapers

Kisa Mdude Chadema, Mbunge Akamatwa Dodoma

Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma jana Jumatatu Mei 6, wakati akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea.

 

Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde amesema hawajapata taarifa rasmi kwanini mbunge huyo amekamatwa. “Huu ni mwendelezo wa matukio ya viongozi wetu kukamatwa, licha kwamba walitakiwa kuujulisha uongozi wa bunge,” alisema Silinde.

 

Inadaiwa Haonga amekamatwa kwa tuhuma za kudai kuwa mpiga kura wake aitwaye Mpaluka Said Nyagali maarufu kama ‘Mdude Chadema’ ametekwa.

Polisi wamesema Haonga anashikiliwa ili aweze kuthibisha madai yake juu ya Mdude kutekwa kwa sababu wao (polisi) hawana taarifa zozote kama Mdude ametekwa.

Comments are closed.