The House of Favourite Newspapers

Kisa pesa ya upatu, Ester Kiama aoga matusi

0

ester-kiama.gifNa Hamida Hassan

Msanii wa filamu Bongo, Ester Kiama amejikuta akioga mvua ya matusi kwa madai kuwa amekuwa akisumbua sana kwenye mchezo wa kupeana pesa ‘upatu’.

Kwenye mchezo huo ambao wamo mastaa mbalimbali akiwemo Jack Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Ester amedaiwa kuwa msumbufu kwenye kuwapa pesa wenzake na baada ya kumvumilia miezi mitatu, hivi karibuni walimuanzishia kwa kumtukana kwenye Mtandao wa Instagram.

“Ester ndiyo tabia yake, tulimvumilia sana mwisho tumechoka ndiyo maana tumeamua kumtukana, mchezo gani mtu unasubiri kila siku na unamuona anaendelea na maisha tu? Kwani mimi hela nilikuwa nachimba?” aliwaka mmoja wa wahanga ambaye alimtaja Ester kama kijumbe.

Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilimwendea hewani Ester ambaye alikana kutukanwa na kudai kuwa aliyetukanwa anajulikana kwani aliwekwa mtandaoni.

Leave A Reply