The House of Favourite Newspapers

Malaika achukulia poa tu video yake kuzuiwa

0

MALAIKAMwanamuziki Diana Exavery ‘Malaika’ awali alichanganyikiwa kufuatia aliyekuwa mpenzi wake, Edward Baruti ‘Eddie’ kushikilia msimamo wake kuwa hawezi kuruhusu video ya msanii huyo ya Wimbo wa Raruararua itoke lakini sasa anachukulia poa tu.

Eddie alifikia uamuzi huo hivi karibuni baada ya kuzinguana na mpenzi wake huyo hivyo kumzuia dairekta wa kichupa hicho, Hanscana kutokitoa mpaka pale atakapoamua yeye kwani ndiye aliyegharamia kila kitu.

Akizungumzia kitendo alichofanya mpenzi wake, Malaika alisema kuwa, mwanzoni kilimuuma lakini sasa hivi anachukulia poa tu akiamini mambo yatamnyookea.

“video yenyewe ilikuwa bomba sana na nilitamani mashabiki wangu waione lakini mpaka sasa haijatoka, naamini mambo yatakwenda sawa soon,” alisema Malaika.

Leave A Reply