The House of Favourite Newspapers

Kisa Simba, Morrison Apewa Mapumziko Maalum Yanga

0

KATIKA kuhakikisha anapona kwa haraka ili arejee uwanjani mapema, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji, Luc Eymael amempa mapumziko ya muda kiungo wake machachari Mghana Bernard Morrison.

 

Mghana huyo alikuwa mfungaji wa bao la ushindi katika Dabi ya Kariakoo iliyowakutanisha Yanga na Simba mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Kiungo huyo katika mchezo huo alishindwa kumaliza ni baada ya kupata maumivu ya goti aliyoyapata siku tatu kabla ya pambano hilo kabla ya kutolewa dakika ya 52.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Morrison alisema kuwa ameanza mapumziko hayo aliyaanza mara baada ya mchezo wa Simba ambao alijitonyesha kabla ya kuomba atolewe kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia.

 

Morrison alisema kuwa, alicheza mchezo huo akiwa na majeraha baada ya yeye kumuomba kocha wake, Luc acheze dakika 45 za kwanza alipoona afya yake imetengemaa baada ya kupatiwa matibabu ya siku ya tatu kuelekea pambano hilo.

 

Aliongeza kuwa anatarajia kukosekana katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC, jana Alhamisi kabla ya Jumapili kujitupa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi kupambana na Namungo FC.

“Nimepewa mapumziko maalum na kocha wa Eymael ni baada ya daktari wa timu kushauri nipumzike kutokana na ukubwa wa majeraha ya goti niliyoyapata kabla ya mchezo na Simba.

 

“Nilipata majeraha hayo nikiwa mazoezini na kupatiwa matibabu ambayo yalinisaidia nicheze kwa dakika hizo nilizozicheza kabla ya kuomba mimi nitolewe kutokana na maumivu niliyokuwa nayasikia.

 

“Daktari alishauri nipumzike kwa hofu ya kuendelea kujitonyesha zaidi wakati tukiwa tunakabiliwa na michezo mingine migumu ya ligi na Kombe la FA ambalo ndiyo tunalitaka tulichukue,” alisema Morrison.

Leave A Reply