The House of Favourite Newspapers

KISA UGONJWA WA MWANAYE… MAMA WEMA AMWAGA MATUSI

MIRIAM Sepetu ambaye ni mama mzazi wa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu juzikati amejivunjia heshima ya kuitwa mama baada ya kumporomoshea ‘mitusi mizito’ mwandishi wetu kisa kuulizwa tu juu ya kilichomsibu mwanaye baada ya video kusambaa ikimuonesha Wema akiingia kwenye hospitali moja iliyopo jijini Dar.

 

Awali baada ya video hiyo kusambaa yaliibuka maneno yaliyozua gumzo kwa wiki nzima iliyopita ikidaiwa kuwa, hali ya Wema siyo nzuri kufuatia kufanyiwa oparesheni na kukatwa utumbo.

Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kufika kwenye hospitali ambayo ilidaiwa staa huyo alikuwa amelazwa lakini madaktari na manesi hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.

 

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti meneja wa Wema, Neema Ndepanya ameulizwa kuhusu kinachomsumbua msanii wake lakini hakuwa tayari kutoa maelezo ya kunyooka licha ya kuwahi kukiri kuwa, staa huyo ana matatizo ya tumbo.

Kutokana na usiri uliotawala kuhusu afya ya Wema, gazeti hili juzi Jumamosi lililazimika kumtafuta mama Wema kupitia simu yake ya mkononi na alipopatikana baada ya kujua kuwa alikuwa akiongea na mwandishi, alianza kuporomosha ‘mitusi mizito’ isiyoandikika gazetini.

 

“Wewe mwandishi……(tusi zito)…. tena nakuambia……. (tusi tena),” alisema mama Wema ambapo baada ya mwandishi kuona anaambulia matusi asiyostahili, ilibidi akae kimya.

Aidha, wakati mama huyo ambaye kwa umri wake na kile alichokuwa akikitoa mdomoni vilikuwa haviendani, akiwa hewani bila kujua kuwa mwandishi hajakata simu, alianza kuwaeleza watu aliokuwa nao kuwa amemkomesha mwandishi.

 

Swali ni je, kulikuwa na ulazima gani wa mama Wema kutukana matusi hayo wakati alichotakiwa kufanya ni kufafanua tu juu ya kile kinacho zungumzwa mitaani kuhusu afya ya mwanaye? Je, kwa matusi hayo atakuwa amepata faida gani kama siyo kuambulia aibu tu? Majibu anayo yeye!

STORI: Memorize Richard, DAR

Comments are closed.