The House of Favourite Newspapers

Kisa Wasauzi… Matajiri Yanga Waweka Mezani Bil 1, Caf Yawaongezea Mkwanja

0

MABOSI wa Yanga wameitengea Marumo Gallants ya Afrika Kusini zaidi ya bilioni moja ili kuimaliza kwa Mkapa.

 

Mei 10, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini na watarudiana Mei 17, mwaka huu huko Sauz.

 

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga jumla ya mabao 2-0 Rivers United, huku Marumo yenyewe ikiwafunga Pramids ya Misri jumla ya mabao 2-1.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limekuwa na kawaida ya kutoa fedha kuanza kwa klabu zinazofuzu hatua ya makundi hadi fainali, kwa hatua waliyofika Yanga wanatarajia kulamba zaidi ya Sh bil 1.

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa, kupitia kikao cha viongozi wa timu hiyo walikubaliana kutumia gharama yoyote hata ikiwa bilioni moja au zaidi ili kuhakikisha wanaweka rekodi ya kucheza fainali msimu huu.

“Ndugu yangu naomba ufahamu kwamba kwenye kikao cha viongozi wamedhamiria kutinga fainali kwa gharama yoyote kwani wamesema wapo tayari kutumia hata zaidi ya bilioni moja kama gharama za kuiwezesha timu kutinga fainali.

“Walisema kama ishu ni kuwafanya wachezaji wawe na furaha ni kuwapa pesa basi watawapa kitita chochote kile ili tu tuweze kutengeneza heshima maana nafasi kama hii huwa ni ngumu sana kujirudia kwenye maisha ya mpira na ndiyo maana wameelekeza pesa zote za Caf zitumike kutufikisha fainali,” kilisema chanzo hicho.

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji ameliambia Championi Jumatano kuwa, watafanya kila jambo kuingia fainali kama walivyofanya kwenye michezo iliyopita kwa kujipanga katika bajeti na maeneo yote wanayoamini kufanikisha hilo.

“Tunatambua wazi kuwa hatua tuliyofikia kwenye Caf ni kubwa na ngumu sana kwetu, ila kwa kuwa tumethubutu na kufanikiwa kufika hapa, basi tutahakikisha tunaingia fainali na kusaka ubingwa huo kwa gharama yoyote ile,” alisema Arafat.

Stori: Musa Mateja

“WAZIRI WALIPENI FIDIA WANANCHI WAMEKUWA WADUMAVU MIAKA 15”-MBUNGE NGONYANI AILIPUA SERIKALI…

Leave A Reply