The House of Favourite Newspapers

Kisa Wimbo, Zuchu, Angella Hapatoshi

0


KWA raha zake Zuchu kaachia ngoma yake iitwayo Nyumba Ndogo ambayo kaipaka mahadhi ya kisingelisingeli. Sasa chawa wa Angella msanii kutoka Konde Gang wamemponda kinomanoma.

 

Wanasema, kitendo cha Zuchu kuimba singeli ni sawa na kukimbilia uhamishoni kwenye ufalme wa akina Mzee wa Bwax; jambo linaloonesha wazi kuwa vita ya muziki wa Bongo Fleva imemshinda; watu wana maneno jamani.

 

Unajua nini kinaendelea hivi sasa? Ni kusagiana kunguni kwa kwenda mbele na kila upande unatumia chawa na silaha zake ambapo sasa Angella anaambiwa anachokitafuta kwa Zuchu atakipata.

 

Heh yamekuwa hayo; lakini yote kwa yote pande mbili zinashindania umalkia kwamba nani kati yao avikwe taji hapa Bongo ni Zuchu wa WCB au Angella wa Harmonize?

 

Wapo wanaosema, Zuchu mkubwa sana kimuziki huwezi kumlinganisha na Angella, lakini wengine wanasema Angella ni moto wa petroli unaowaka. Wewe mdau wa falme hii ya Instagram unampa nani kura yako?

STORI NA RICH MANYOTA | GPL

Leave A Reply