The House of Favourite Newspapers

KISS DANIEL ABADILI JINA

Daniel Anidugbe ‘Kiss Daniel’

MKALI wa Ngoma ya No Do na Sofa, Oluwatobiloba Daniel Anidugbe ‘Kiss Daniel’ amebadilisha jina na kuanza kujiita Kizz Daniel.

Ishu hiyo imekuja kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa kibiashara kati yake na lebo ya muziki ya zamani ya G-Worldwide iliyokuwa ikisimamia kazi zake ambapo ilifikia hatua ya kumburuza mahakamani kwa madai kuwa amekiuka na kushindwa kutimika vigezo na msharti ya mkataba wa kibiashara waliokuwa wamesaini kisha wakamtaka asitumie jina la Kiss Daniel kwa kuwa ni mali yao.

Kiss Daniel, baada ya kuvunjika kwa mkataba wake na G-Worldwide alianzisha lebo yake iitwayo FLY BOY I.N.C ambapo ameshabadili jina na kuwa Kizz Daniel.

Hata katika mitandao yake ya kijamii, tayari ameshaanza kupatikana kwa jina hilo jipya.

 

LAGOS, Nigeria

Comments are closed.