The House of Favourite Newspapers

Kiungo Matata Yanga Atangaza Hali ya Hatari

Mohammed Issa ‘Banka’

KIUNGO matata wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’ ambaye alifungiwa asicheze soka kwa miaka miwili ameibuka na kutamba yuko fiti kutokana na mazoezi anayoendelea kuyafanya.

 

Mo Banka licha ya kusajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, hadi sasa hajaichezea timu hiyo kutokana na kufungiwa kwa tuhuma za kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.

 

Kiungo huyo ambaye ameandaliwa kuvaa jezi namba 8 ndani ya Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa yuko fiti baada ya kuanza kufanya mazoezi ya muda mrefu katika kikosi hicho kinachofundishwa na Mkongomani, Mwinyi Zahera.

 

“Mbona mimi nimeshaanza mazoezi siku nyingi kwenye timu yangu ya Yanga, nipo fiti kabisa na nikianza kukipiga uwanjani kila mmoja atashangaa, subirini moto wangu,” alisema Mo Banka akizungumzia juu ya maandalizi yake wakati huu ambao adhabu yake inaenda kumalizika.

 

Kiungo huyo atarejea dimbani kwa mara nyingine mara baada ya adhabu yake kumalizika Februari 8, mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mechi dhidi ya Simba itakayopigwa Februari 16, mwaka huu.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.