The House of Favourite Newspapers

Kiungo Mkenya Asepa Azam

0

KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Azam, Kenneth Muguna leo Jumatatu anatarajiwa kuanza safari ya kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo Ndola, Zambia kurejea kwao kujiunga na kikosi cha timu yao ya taifa.

 

Azam ipo Ndola, Zambia kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ya takribani wiki moja na nusu, ambapo wakiwa huko wamepanga kucheza michezo minne ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania Septemba 5, mwaka huu.

 

Watakaporejea Azam watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, unaotarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ hapa Ndola Zambia ambapo leo (jana), Jumapili tutacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kabwe Warriors ambao utakuwa ni mchezo wa pili kati ya michezo minne ya kirafiki tuliopanga kucheza.

 

“Baada ya mchezo huu tunatarajia kuwa kiungo wetu wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna ataondoka kambini kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya nchi yao.”

Joel Thomas, Dar es salaam

Leave A Reply