The House of Favourite Newspapers

Kiungo Mnigeria Afunguka Yaliyojiri Simba

0

KIUNGO Mnigeria, Udoh Etop David, amethibitisha kwamba, hajafanikiwa kupata mkataba wa kuitumikia Simba baada ya kufanya majaribio kwa takribani wiki moja.


Udoh akiwa kwenye
majaribio hayo, alifanikiwa kucheza mechi mbili za Kombe la Mapinduzi, lakini ameshindwa kumshawishi Kocha Pablo Franco.


Akizungumza na Spoti
Xtra, kiungo huyo mkabaji, alisema licha ya kutarajia kupewa makataba na timu hiyo, lakini hajafanikiwa na kwa sasa kitu ambacho anatarajia ni mipango ya safari yake kutoka Tanzania kurudi kwao Nigeria.


“Maisha ya Tanzania ni
mazuri na nimeyapenda sana, ndani ya Simba nimekaa vizuri kuanzia kambini hadi kwenye mechi.


“Kuhusu kupewa
mkataba na Simba hapana,hakuna maisha mengine tena ndani ya Simba.

“Kwa sasa naangalia mipango yangu ya kuondoka Tanzania kurudi nyumbani Nigeria na leo (jana) Jumamosi
naenda kupima vipimo vya
Corona, kisha nitaondoka,” alisema mchezaji huyo.

STORI: MARCO MZUMBE

Leave A Reply