The House of Favourite Newspapers

Kiungo Mpya Ajiondoa Simba Arejea Nyumbani Kwao, Uongozi Wafunguka

0

UONGOZI wa Simba, upo katika mipango ya kumruhusu kiungo wao, Muivory Coast, Aubin Kramo, kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu ya majeraha yake ya goti.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo, ajitoneshe majeraha hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome FC uliochezwa Simba Mo Arena, Bunju, Dar, wikiendi iliyopita.

Katika mchezo huo, Simba walibuka na ushindi wa mabao 6-0 ambao kiungo huyo alitolewa katika dakika 42 baada ya kujitonesha jeraha hilo linalomsumbua tangu ajiunge na timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo huyo juzi alikutana na uongozi wa timu hiyo, na kuomba arejee kwao kwa ajili ya matibabu hayo ya goti.

Mtoa taarifa huyo alisema, uongozi unafikiria kumruhusu kiungo arejee kwao, licha ya hivi sasa kusubiria vipimo vya MRI, ili kufahamu ukubwa wa tatizo lake.

“Jeraha hilo la goti limekuwa likimsumbua mara kwa mara tangu Kramo ajiunge na timu, hivyo hivi sasa yupo katika mazungumzo na uongozi kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwao kujitibia.

“Mara ya pili Kramo anakaa nje ya uwanja kutokana na jeraha hilo la goti ambalo limekuwa likimtesa, hivyo ameona ni bora akarejea kwao kwa ajili ya kwenda kujitibia.

“Anachosubiria ruhusa ya viongozi pekee ambayo itamfanya arejee haraka nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu wakati huu akisubiria majibu ya vipimo baada ya juzi kufanyiwa ambayo yatatoka kesho (leo) Jumanne,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alithibitisha kupata majeraha kwa kiungo huyo akisema: “Ni kweli Kramo alipata majeraha ya goti, hivi sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari akiendelea kupatiwa matibabu kuhakikisha anarejea haraka uwanjani.”

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Tunasikitika kuona mchezaji wetu muhimu kaumia kwa mara nyingine, tunangojea ripoti ya madaktari halafu tutawajulisha ni kwa namna gani ataendelea kusubiria.

“Uhakika ni kwamba hakupata majeraha makubwa sana safari hii, hivyo yawezekana akawa hajaumia ki hivyo au madaktari wao ndio watasema nini kitajiri baada ya kupata dhuruba hiyo,” alisema.

STORI NA WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

#EXCLUSIVE: MTOTO GENIUS ANAYEWASHINDA HADI WANAFUNZI wa FORM 4, HUWEZI KUAMINI BADO HAJAANZA SHULE

Leave A Reply