The House of Favourite Newspapers

Knauf Tanzania Yatoa Misaada Wilayani Kilwa

0
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited wakifurahi na wanafunzi wa shuke ya msingi Kiranjeranje iliyopo Kilwa mkoani Lindi muda mfupi baada ya kampuni hiyo kutoa msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo. Kampuni hiyo pia ilitoa madawati 100 kwa shule ya msingi Makangaga,kisima cha maji katika Kijiji cha Makangaga na pedi za kike katoni 16 kwa shule ya sekondari Kiranjeranje.

 

 

 

Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited leo imekabidhi kisima cha maji kwa wakazi wa Kijiji cha Makangaga na kutoa jumla ya madawati 200 kwa shule za msingi Makangaga na Kiranjeranje zilizopo wilaya yaKilwa, mkoani Lindi.

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashari wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited Ilse Boshoff (kulia) akimsiliza mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiranjeranje Elibariki Kululinda (kushoto) muda mpupi kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo. Katikati ni meneja rasilimali watu wa kampuni hiyo Rose Mero. . Kampuni hiyo pia ilitoa madawati 100 kwa shule ya msingi Makangaga,kisima cha maji katika Kijiji cha Makangaga na pedi za kike katoni 16 kwa shule ya sekondari Kiranjeranje.

 

 

 

Kampuni hiyo pia imetoa katoni 16 za pedi za kike kwa shule ya sekondari Kiranjeranje, msaada ambao utasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa kike ambao hushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited wakiongozwa na Mkurugenzi wao wa kanda ya Afrika Mashariki Ilse Boshoff (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, walimu na viongozi wa shule la msingi Kiranjeranje na Makangaga pamoja na viongozi wa elimu wa wilaya ya Kilwa muda mfupi baada ya kutoa msaada wa kisima, madawati na pedi za kike.

 

 

Kisima kilichokabidhiwa kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 2,000 na kinatarajiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama ambayo ilikuwa inawakabili wakazi wa Makangaga waliolazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu.

 

 

Akiongea wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Knauf kanda ya Afrika Mashariki Ilse Boshoff, alisema kampuni hiyo ambayo ina migodi ya kuchimba gypsum katika vijiji husika imeamua kutoa misaada kwa wakazi wa vijiji hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

 

“Mradi huu wa maji siyo tu  utaboresha afya za wakazi wa Makangaga bali pia utasaidia shughuli za uzalishaji mali, haswa kwa wanawake na wasichana ambao hutumia muda mrefu kwenda kutafuta maji na badala yake wasichana watapata muda wa kuhudhuria masomo yao na wanawake kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi,” alisema.

 

Kwa upande wa msaada wa madawati alisema ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule hizo mbili.

 

“Tumeamua kutoa msaada wa madawati kwakuwa tunajua umuhimu wa elimu kwa maendeleo.

Kupitia madawati haya tunaamini kuwa wanafunzi wataweza kujifunza katika mazingira bora zaidi,”

 

Akitoa shukrani zake kwa misaada hiyo, mwenyekiti wa halmashauri ya Kilwa, Eston Ngilangwa aliishukuru kampuni ya Knauf kwa misaada hiyo na kusema msaada wa madawati umekuja wakati muafaka kwakuwa shule zilizonufaika zilikuwa zinakabiliwa na uhaba wa madawati.

 

Kuhusiana na mradi wa maji alisema Maji ni uhai, tunawashukuru Knauf kwa kutuletea uhai.

 

Wakina mama na wasichana ambao walikuwa na mzigo wa kutafuta maji kwaajili ya familia sasa watapata huduma hii muhimu jirani na maeneo wanayoishi.”

 

Leave A Reply