The House of Favourite Newspapers

Zari: Wenye Wivu Wajinyonge

0

PAMOJA na kukanusha mara kadhaa akisema wao ni marafiki tu, hatimaye mwanamama Zari The Boss Lady amechoka kufichaficha kwani penzi ni kikohozi na kulificha huwezi! Hatimaye Zari ameamua kujilipua waziwazi kuwa mwanaume ambaye anaonekana wakiwa pamoja mara nyingi ndiye mpenzi wake kwa sasa; yaani kipende roho huku timu yake ikisisitiza;

“Habari ndiyo hiyo, wenye wivu wajinyonge!” Ikumbukwe Zari ni mzazi mwenza wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye wamebahatika kupata watoto wawili; Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Wikiendi iliyopita, Zari na mwanaume wake huyo wameendelea kuchafua mitandao ya kijamii kutokana na kuenelea kusambaa kwa picha zao za kimahaba wakila bata zilizokwenda shule. Katika picha nyingi mitandaoni, Zari anaonekana kwenye picha mbalimbali na mwanaume huyo ambaye majasusi wa mitandaoni wamemtambua kwa jina la GK Choppa ambaye ni Mganda anayesemekana kumpokea Zari jijini Durban nchini Afrika Kusini.

Zari ameendelea kuibua gumzo wakati huu baada ya kumuanika mwanaume huyo ambaye amekuwa akijiachia naye huku kukiwa na madai yaleyale kwamba naye ni mdogo kiumri (kiben’teni). Picha za kumwaga za kimahaba zimefanya baadhi ya wafuasi wa Zari wapatao zaidi ya milioni 10 kuamini kwamba Zari yupo kwenye mahaba mazito na jamaa huyo.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanasema kuwa, Zari amefikia hatua hiyo ya kumtangaza mpenzi wake huyo baada ya kushindwa kuhimili kishindo cha tetesi za Diamond kutoka kimapenzi na msanii wake, Zuchu. Kadiri habari za Diamond na Zuchu zilivyoendelea kushika kasi, ndivyo habari za Zari na mwanaume huyo nazo zinashika kasi. Wengine wanaamini kuwa, Zari anafanya hivyo kupooza maumivu ya Diamond na Zuchu kwani huwenda aliamini jamaa huyo angerudi kwake.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply