The House of Favourite Newspapers

Kocha AS Vita Awapa Angalizo Simba, Yanga Michuano ya Kimataifa

0
Roul Shungu

KOCHA Msaidizi wa AS Vita ya DR Congo, Roul Shungu, amefunguka kuwa, Simba na Yanga zina uwezo wa kufika mbali msimu huu katika michuano ya kimataifa ikiwa watazingatia malengo na mipango yao licha ya kupangwa kwenye makundi magumu.

Shungu ametoa kauli hiyo baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupanga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo iliyochezeshwa juzi nchini Afrika Kusini.

Katika droo hiyo, Simba imepangwa Kundi B na timu za Wydad Casablanca, Jwaneng Galaxy na ASEC Mimosa, wakati Yanga ikiwa Kundi D na timu za Al Ahly, CR Belouizdad na Medeama.

Akizungumza na Spoti Xtra, Shungu alisema Yanga na Simba wana nafasi kubwa ya kupiga hatua ya kusonga mbele katika michuano hiyo ikiwa watazingatia mipango na malengo yao katika michuano hiyo licha ya kupangwa na timu ngumu.

“Unaweza kuwa msimu mgumu kwa kwa timu zote mbili, lakini bado naamini kama watajipanga basi wana kila sababu ya kufika robo fainali ikiwa watafanya mambo kwa malengo yao pasipokuwa na presha kwa sababu ukiangalia kwa namna makundi yao yalivyo hakuna mwenye nafasi kutokana na kila mmoja kumuhofia mwenzake.

“Wana kila sababu ya kufanya vizuri maana timu zote zina uzoefu wa kutosha wa kufanya makubwa kutokana na ushiriki wao katika michuano hii mikubwa ambayo ukiangalia Yanga wamecheza fainali ya Shirikisho msimu uliopita na Simba wakiishia  robo fainali, hivyo kila mmoja anayo nafasi ya kwenda mbele kupiga hatua,” alisema Shungu.

Leave A Reply