The House of Favourite Newspapers

Kocha Aussems Akwea Pipa na Kusepa Zake – Video

0

HATIMAYE aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameondoka nchini Tanzania na kurejea nyumbani kwao baada ya Timu hiyo kusitisha mkataba wake hivi karibuni.

 

Aussems ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku ambapo kabla ya kukwea pipa alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya mwisho na vyombo vya habari.

“Asanteni mashabiki na wachezaji kwa ushirikiano wenu, nawatakia kila la heri! Lakini ili Simba iimarike kwenye bodi lazima iondokane kabisa na waongo na wasio na elimu. Sasa ni muda kwangu kufurahia kitu muhimu kwenye maisha, familia na watu wakweli,” amesema Aussems.

Leave A Reply