The House of Favourite Newspapers

Kocha Mpya wa Simba ni Patrick Aussems Kutoka Ubelgiji

Patrick Aussems.

VIONGOZI timu ya Simba wameamua kumshusha kimyakimya siku ya Jumapili kocha Patrick Aussems kutoka Ubelgiji ili kufanya mazungumzo ya kuchukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre, waliyeachana naye mwezi uliopita baada ya kuinoa timu hiyo kwa miezi sita tu.

 

Kocha huyo yupo katika mazungumzo ya mwisho na  viongozi wa Simba kabla ya kupewa kazi ya kuinoa timu hiyo itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

 

Patrick Winand Aussems alizaliwa, Februari 6, 1965 katika mji wa Moelingen, Ubelgiji na kuichezea RCS Vise kati ya 1974-81, klabu iliyokuja kufilisika mwaka 2014. Patrick alikipiga pia Standard Liege (1981-88), kisha kutua K.A.A Gent (1988-19), R.F.C Seraing (1989-90) na ES Troyes AC (1990-93).

 

Baada ya kustaafu mwaka 1993 kama kocha/mchezaji wa Troyes inayoshikilia Ligue1, alijitosa jumla kuwa kocha ndani ya klabu hiyo hadi 1995 alipotua Saint Lousienne ya Re Union.

Comments are closed.