The House of Favourite Newspapers

Kocha Mrundi Ataja Sifa Tano za Kagere

0

HITIMANA Thierry, Kocha Mkuu wa Namungo FC ambaye ni raia wa Burundi, amesema kuwa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ana sifa tano ambazo ni muhimu kwa mshambuliaji kuwa nazo.

 

Kagere alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Gor Mahia ya Kenya, msimu wake wa kwanza alinyanyua makwapa kubeba mataji mawili ambayo ni Ligi Kuu Bara na Ngao ya Jamii.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Thierry alisema kuwa mshambuliaji makini ni yule mwenye mwendelezo mzuri na anatimiza majukumu kwa wakati.

 

“Kagere nimemtazama ni aina ya washambuliaji ambao siyo wepesi kukata tamaa, ana spidi akiwa ndani ya uwanja, uwezo wa kukaba, uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi, hivi ni vitu vya msingi kwa mshambuliaji kuwa navyo.

 

“Ninaamini kama ligi ingekuwa inaendelea tungeshuhudia mengi na kwenye upande wa washambuliaji waliokuwa wanapambana nao yupo na kijana wangu Reliants Lusajo, naye ni mpambanaji, pia ninaamini kuna vitu anajifunza kutoka kwa Kagere,” alisema.

 

Msimu huu katika Ligi Kuu Bara, Kagere amefunga mabao 19 na ametoa pasi tano za mabao, msimu wake wa kwanza alifunga mabao 23 na alikuwa ni mfungaji bora.

Stori Lunyamadzo Mlyuka,Dar es Salaam

Leave A Reply