The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Aichimba Mkwara Azam

0

KOCHA wa Simba, Didier Gomes ameichimba mkwara Azam FC kuelekea kwenye mchezo wao wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam unaotarajiwa kupigwa leo kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Songea.

 

Mchezo huo wa kihistoria ambao ni muhimu kwa timu kupata ushindi ili ifuzu hatua ya fainali ambayo bingwa atakata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika, mwakani.

Timu hizo katika mchezo wa mwisho kukutana kwenye Ligi Kuu Bara ni Februari 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

 

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kikubwa wanataka kufuzu kucheza fainali.

 

Gomes alisema kuwa malengo yao katika msimu huu ni kutetea mataji yote wanayoyashikilia kwa kuanzia ligi na Kombe la FA, hivyo ni lazima wawafunge wapinzani wao Azam.

“Lazima kesho (leo) tuonyeshe tunataka kufika fainali kwa kujituma na kuonyesha uwezo.

 

Lazima tuchukue ubingwa wa ligi na lazima tuchukue FA. “Tunawaheshimu Azam, ni timu kubwa na ngumu ambayo tulikutana nayo katika ligi, lakini licha ya ukubwa wao lazima tuwafunge ili tucheze fainali,” alisema Gomes.

 

Kwa upande wa nahodha wa timu hiyo, John Bocco, alisema kuwa: “Tunaenda kukutana na timu nzuri, tunawaheshimu kwa hilo lakini tumejipanga vizuri na Mungu atatusaidia kupata matokeo mazuri na kufuzu fainali.”

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

KUFURU ya IRENE UWOYA! AMWAGA PESA kama ZOTE HARUSI ya DIDAH

Leave A Reply