The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Aungana na Global Dhidi ya Corona – (Picha +Video)

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (kulia),  akimkabidhi misaada mlezi wa kituo cha yatima Sinza, Hassan Hamisi,  Aprili 23, 2020 katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya misaada iliyotolewa.

MKURUGENZI Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo leo Aprili 23, 2020 ametoa pongezi kwa kocha wa zamani wa Simba, Talib Hilal, ambaye amevutiwa na namna ambavyo Global Group imekuwa ikisaidia jamii na hivyo kuamua kushirikiana nayo katika kufikisha misaada kupitia kampuni hiyo iliyopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa Talib ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni la Oman na safari hii ametoa msaada wa vyakula ambavyo ni pamoja na  sukari, mchele, tambi na mafuta katika vituo vinne vya watoto yatima jijini Dar es Salaam na kimoja jijini Mwanza.

 

Kocha huyo aliyekuwa pia mchezaji wa zamani wa Simba aliamua kufanya hivyo kwa kuwa lilikuwa lengo lake siku nyingi lakini hakuwa amepata wa kushirikiana naye kufikisha misaada yake.

 

“Nilipoona Global mnasaidia watu mitaani, nikaona ni watu ambao ninaweza kushirikiana nao kufikisha hiki nilichonacho  kupitia kampuni hii kwa ajili ya Watanzania na hasa sasa ambapo ni mwezi wa Ramadhani.  Nashukuru sana,” alisema Talib.

 Mlezi wa kituo cha yatima Sinza, Zaidia Nuru Hassani, akipokea misaada kutoka kwa Shigongo.

Kabla ya hapo, kwa kushirikiana na Global Group pia, Talib alitoa ndoo na sabuni kwa vituo vinne vya watoto yatima, lengo likiwa kuwasaidia kujikinga na maambukizi dhidi ya Corona.

 

Baada ya hapo, akatoa ndoo  na sabuni pia kwa madereva wa Bajaj na Bodaboda kwa kuwa wamekuwa wakitoa huduma kwa watu.

 

Misaada yake yote imekuwa ikifikishwa na Global Group ambayo awali ilianza kusaidia watu mbalimbali katika jamii na kumvutia kocha huyo.

Waliopewa misaada wakiondoka katika ofisi ya Global Group baada ya kukabidhiwa.

Leave A Reply