The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba: Tutarudi Tukiwa Bora Zaidi

0

KOCHA wa viungo wa klabu ya Simba, Adel Zrane amefunguka kuwa kipigo walichopata dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kimewaumiza, lakini hawawezi kurudi nyuma bali watarekebisha makosa yao na kurejea wakiwa bora zaidi.

Simba Jumamosi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, walikubali kipigo cha bao 1-0, na kuvuliwa rasmi ubingwa wa Ngao ya Jamii ambao waliutwaa kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.

Hicho ni kipigo cha pili mfululizo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo walianza kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kilele cha siku ya Simba ‘Simba Day’, kabla ya Jumamosi kufungwa tena na Yanga.

Simba leo Jumanne wataanza rasmi michezo yao ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2021/22 ugenini dhidi ya Biashara United, mkoani Mara.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Zrane alisema: “Kama benchi la ufundi tumeumizwa sana na matokeo ya mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Yanga, kupoteza mchezo na kupoteza taji halikuwa jambo rahisi kwetu na kwa mashabiki wetu.

“Lakini kila mtu anajua kuwa kuna wakati mpira unakuwa na matokeo ya tofauti na matarajio, hivyo tumepata funzo na tutakaa chini na kufanyia kazi upungufu ambao ulijitokeza kwenye mchezo ule, na kuurekebisha kisha tutasonga mbele.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply