The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi Ampeleka Okrah Ufukweni

0

KATIKA kuhakikisha kuwa Yanga inarudi ikiwa na makali yake yale yale kwenye michuano ya kimataifa na ligi kuu, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ameanza tizi kwa kuwapigisha mastaa wake akiwemo Augustine Okrah tizi la maana Fukwe za Coco jijini Dar.

Ikumbukwe Yanga walikuwa na mapumziko ya siku kadhaa baada ya kumalizika kwa Mapinduzi Cup huku Januari 16 wakirejea na kuanza mazoezi rasmi.

Championi Ijumaa lilishuhudia mazoezi ya Kocha Gamondi na mastaa hao ambao waliweza kufanya mazoezi mbalimbali kama kukimbia wakifanya hivyo kwa dakika 40, kuchezea mpira na yale ya viungo kwa zaidi ya saa moja na nusu.

Baadhi ya mastaa waliokuwepo mazoezini hapo ni Okrah, Shekhan Hamisi huku wengine wakiwa ni Pacome Zouzou, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Kibwana Shomari, Clement Mzize, Zawadi Mauya, Jonas Mkude, Yao Khouas Attouhula, Gift Fred, Farrid Mussa, Joyce Lomalisa na Skudu Makudubela.

Stori na Marco Mzumbe

MUSONDA AFUNGUKA WALICHOKIFANYA na CHAMA BAADA ya KUINGIA na KUFANIKIWA KUPATA SARE..

Leave A Reply