The House of Favourite Newspapers

Kopa Kushuka na T.O.T Taarab Dar Live

 

Mwandishi Wetu | CHAMPIONI| Dar es Salaam

ZIKIWA zimesalia wiki kadhaa kufikia Sikukuu ya Pasaka, Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa ameweka wazi kuwa siku hiyo atashuka kwa mara nyingine na bendi yake ya Taarab, T.O.T ndani Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kopa ambaye ni mkongwe wa muziki huo akiwa na nyimbo kibao kama vile Magumegume na Full Stop alisema, siku zote T.O.T Taarab huwa haiwaangushi mashabiki wake, hivyo waje washuhudie sapraiz ya nyimbo zao mpya watakazoimba kwa mara ya kwanza Dar Live.

“Siku zote sina maneno mengi, tukutane Dar Live nikiwa na T.O.T Taarab,” alisema Kopa.

Naye Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo mbali na uwepo wa Kopa, kutakuwa na wakali wengine kibao kama Harmorapa, Juma Nature, Msaga Sumu, Dullah Makabila na Pambano la Ngumi.

“Mapema kuanzia asubuhi kutakuwa na Makhirikhiri wa Tanzania ambapo watoto watapata fursa ya kujiachia kwa kushiriki michezo mbalimbali ambayo tumewaandalia,” alisema Mbizo.

Comments are closed.