The House of Favourite Newspapers

Viwanja Vya Ugenini Vinaboresha Viwango

Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| LOVE SMS

HALO HALOOOOO, mashostito, mnaendeleaje na kazi lakini? Mwenzenu sijambo, nipo zangu barazani kama kawa, kazi yangu kubwa umbeya malipo kwa Mungu, unadhani binadamu gani atakulipa kwa umbeya kama siyo kuitiwa kigodoro?!

Hata hivyo, lakini nashukuru, maana nimekuwa nikipokea simu kutoka kwa mashangingi wenzangu wastaafu walioko huko mikoani, wakiniambia eti mada mnazotaka tuziongelee zina mashabiki sana. Ni kweli wajameni? Haya.

Basi juzi nimekaa barazani kwangu mpweke, mara kaja Mwantum, yule binti wa Kizanaki alokua akikaa mtaa wa pili akaolewa kule kwa kina Mwanakombo, mwenyewe  ‘bebi’ wako akuambie mwende zenu mkakae hoteli ukatae?

Sasa nikamwuliza Mwantum, kama hivyo hutaki, je huwa mwenzio anakutoaga out? Akasema hilo pia analazimishwa, yeye hapendi ingawa anatokaga mara moja moja, ila hapendi kwenda mbali na nyumbani kwake, wakitoka wakakaa hapo baa ya jirani, apate zake nyama choma na kabia kamoja, basi inatosha!

Mh, nisiwe mnafiki, huyu mume ningempata mie, mbona wachonga midomo ingewakauka? kanuna, nikamuuliza vipi tena nyumba inawaka moto, akatingisha kichwa kukataa, sasa kulikoni? Akanistaajabisha, eti anakerwa na mumewe, muda mrefu anamsumbua, anataka siku moja kwa mwezi watoke wakakae hoteli, wafanye yao warejee kesho yake.

Eti yeye anaona jambo hilo halina maana, na tena ni kupoteza bure pesa, hasa wakati wenyewe mgumu kama huu! Jamani, mie hata sijui nianzaje, lakini niwaambie wazi, kama zile enzi zetu, mbona tungepiga ngoma kusherehekea?

Yaani aniambie mama tutoke mie nilete nyodo, eti mama twende tukapumzike hapo Atriums hotel, mie nianze kuumauma kucha? Weee nani kakuambia, mie huyuhuyu Anti Nasra, labda nimerogwa! Sasa usicheke kwa hisia zangu, nataka nikuambie jambo la kweli, asikudanganye mtu, mechi za ugenini zinaongeza viwango vya uchezaji.

Wee fikiria mwenyewe, kila siku upo katika uwanja huo huo, unajua magoli yalivyokaa, upande gani upo bondeni na hata yalipo mashimo, uchezaji wake utakuwa ule ule, kwa sababu unajua ukifika pale, pako hivi. Viwanja vya ugenini ni muhimu sana kwa ajili ya kupandisha viwango vya mchezo, kwa kila mchezaji, iwe wewe au mwenzio.

Unapokutana na mazingira mapya, kwanza utacheza kwa tahadhari, unaweza kugundua kuwa ule uwanja unaocheza wa ugenini- ni mbovu kuliko wako wa nyumbani, kwa hiyo unatengeneza nafasi ya kujiamini katika game! Timu haiwezi kupandisha kiwango chake kama kila siku inachezea uwanja wake wa nyumbani tu, lazima itoke, ikutane na uwanja tofauti, hali ya hewa tofauti na mashabiki tofauti.

Timu inapoweza kushinda mbele ya halaiki ya kigeni, inazidi kujiamini na ndiyo maana unakuta zingine huwa hazifungiki katika uwanja wao wa nyumbani kwa vile wana uzoefu wa kutosha. Ukipata fursa ya kutoka, nenda shoga.

Ni vizuri kama mkajenga mazoea ya kufanya hivyo mara kwa mara, kwanza yanaboresha penzi lenu, maana kukaa sana nyumbani, wakati mwingine hasira za kuudhiwa na watoto nazo zinachosha eti, mkitoka na kukaa peke yenu, mtaongea yanayowahusu tu, ambayo wakati mwingine mnakosa nafasi mkiwa nyumbani!

 

Comments are closed.