The House of Favourite Newspapers

Kopa: Nitashuka na T.O.T Taarab Dar Live

Khadija Kopa akiwa jukwaani.

Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

ZIKIWA zimesalia wiki kadhaa kufikia Sikukuu ya Pasaka, Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa ameweka wazi kuwa siku hiyo atashuka kwa mara nyingine na bendi yake ya Taarab, T.O.T ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Vibes, Kopa ambaye ni mkongwe wa muziki huo akiwa na nyimbo kibao kama vile Magumegume na Full Stop alisema, siku zote T.O.T Taarab huwa haiwaangushi mashabiki wake hivyo waje washuhudie sapraizi ya nyimbo zao mpya watakazoimba kwa mara ya kwanza Dar Live.

“Siku zote sina maneno mengi, tukutane Dar Live nikiwa na T.O.T Taarab,” alisema Kopa. Naye Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo mbali na uwepo wa Kopa, kutakuwa na wakali wengine kibao kama Harmorapa, Nature, Msagasumu, Dulla Makabila na Pambano la Ngumi.

“Mapema kuanzia asubuhi kutakuwa na Makhirikhiri wa Tanzania ambapo watoto wote kwa pamoja watapata kujiachia kwa michezo ya kuogelea, kucheza kwenye treni, ndege na mashindano mbalimbali,” alisema Mbizo.

Comments are closed.