The House of Favourite Newspapers

Kotei: Msuva Nenda Zako Ulaya

Omary Mdose na Musa Mateja | CHAMPIONI| Dar es Salaam

KIWANGO alichokionyesha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Simba, kimemkosha kiungo wa Simba, James Kotei raia wa Ghana ambaye baada ya kumalizika kwa mchezo huo walifanya kikao cha dharura.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kumalizika kwa Simba kushinda kwa mabao 2-1, Msuva ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga huku yale ya Simba yakifungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya.

Akizungumzia kikao hicho cha dharura, Msuva alisema, alifuatwa na Kotei na kumpongeza kwa kucheza kwa juhudi kubwa huku akimwambia kwa kiwango chake hastahili tena kubaki Tanzania kucheza soka.

“Unajua baada ya kufungwa niliishiwa pozi kabisa, nikawa nimekaa tu uwanjani, ghafla akaja Kotei na kuanza kunipongeza kutokana na kiwango nilichokionyesha siku ile, aliniambia ni muda muafaka wa mimi kwenda kucheza mbele katika mataifa ya Ulaya na si kuendelea kubaki Tanzania,” alisema Msuva. Naye Kotei aliliambia Championi Jumatano kuwa:

“Nimevutiwa na kiwango cha yule mchezaji wa Yanga anayevaa jezi namba 27 (Msuva), kwani alikuwa akitusumbua sana kuliko wachezaji wengine wote wa Yanga. “Naweza kusema licha ya kuwafunga, lakini Yanga ilikuwa na mchezaji mmoja tu uwanjani kwa muda wote wa dakika tisini ambaye ni yeye.”

Comments are closed.