The House of Favourite Newspapers

Kotei: Yanga Wagumu Ila Watalainika Tu

STORI NA HADJA MGWAI| CHAMPIONI JUMAMOSI |

KIUNGO wa Simba, James Kotei raia wa Ghana amesema kweli kwamba Yanga ina kikosi kizuri lakini haiwezi kuwa sababu ya wao kutoifunga watakapokutana Februari 25, mwaka huu. Simba na Yanga zitacheza mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara Jumamosi ya wiki ijayo baada ya awali Oktoba Mosi, mwaka jana kutoka sare ya bao 1-1.

Hadi sasa Simba imeshinda mechi tatu mfululizo ambapo mbili ni  za ligi kuu dhidi ya Majimaji (3-0) na Prisons (3-0) na ile ya juzi Alhamisi ya 16 Bora ya Kombe la FA dhidi ya African Lyon iliyoshinda kwa bao 1-0. Kotei aliliambia Championi Jumamosi, kuwa amefurahishwa kuona wamefanikiwa kuongoza katika ligi na kusonga mbele katika Kombe la FA na sasa wanachowaza ni mechi yao dhidi ya Yanga wiki ijayo.

“Nimefurahi kuona tumefanikiwa kushinda mchezo huu na kuweza kuongoza katika ligi, ligi ni ngumu hivyo tunahitaji
kupambana ili kuweza kufanikiwa kushinda kila mechi ili tuwe mabingwa.

“Mchezo wetu na Yanga utakuwa mgumu, hivyo tunahitaji kujituma ili kuweza kufanikiwa kushinda mechi hiyo, Yanga ni timu nzuri, nilijifunza vitu vingi nilipokutana nayo kwa mara ya kwanza Zanzibar.

“Nikipata nafasi ya kucheza siku hiyo, nitajitahidi kupambana ili kuipa ushindi Simba lakini kocha ndiye anayeamua ila yeyote atakayecheza naamini ataibeba Simba,” alisema Kotei.

Comments are closed.