The House of Favourite Newspapers

Kumbe kifaa cha Nuh Mziwanda ni Mnyalukolo

0

Nuh-mziwandaImebumburuka! Kumbe ‘kifaa’ kipya cha msanii wa Bongo Fleva,  Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, kinachojulikana kwa jina moja la Erah ni Mnyalukolo wa mkoani Iringa.

Chanzo kilimwaga ubuyu kuwa kifaa hicho kina asili ya Tanzania asilimia zote na kwamba hakitoki Uarabuni kama wengi wanavyofikiria.

“Nyie hamjui tu, mchumba mpya wa Nuh wala siyo Mwarabu wa Dubai kama wanavyojisifu ni Mnyalukolo tii namjua sana yule,” kilisema chanzo.

Showbiz Xtra kama kawa ilimnyanyulia waya Nuh na kumuuliza kama kuna ukweli ambapo alifunguka;

“ Ahaa, nyie bwana! Ni kweli demu wangu ni Mtanzania halisi na ni kweli tena nimetoka naye mkoa mmoja ambao ni Iringa.”

Awali Nuh alikuwa akitoka na msanii wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole.’

Leave A Reply