The House of Favourite Newspapers

Kunywa Juisi Hii Kukuza Nywele Zako

KAMA una tatizo la nywele zako kutokuwa vizuri au kukatika kwa nywele zako, unaweza kuzikuza na kuziweka sawa kwa kutumia juisi hii ambayo unaweza kutengeneza nyumbani.

JUISI YA KWANZA

Nusu tango, karoti 5 kubwa, tufaha moja kisha saga kunywa utaona jinsi nywele zako zitakavyokuwa fasta.

JUISI YA PILI

Juisi nyingine ni mcha-nganyiko wa robo tango, karoti kubwa 4 na nyanya, saga kisha kunywa, hii itakusaidia kwani inakuza nywele kuanzia kwenye mizizi.

JUISI YA TATU

Juisi nyingine ni ya nusu kiazi damu, karoti 5 kubwa na nusu tango moja, saga kisha kunywa.

Kunywa juisi hizi kwa wiki mara mbili kama unao uwezo ingawa kama unaweza kupata matunda haya kunywa hata kila siku iwe sehemu ya mlo wako, itakusaidia kukuza nywele.

Comments are closed.