The House of Favourite Newspapers

Kuoa wake wanne sawa, lakini mpe mkeo haki yake!

0

15_forgotten_habits_of_happy_couples_01Asalam alaikum wapenzi wasomaji wangu wote ambao mmekuwa pamoja katika mada zangu ninazotoa kila wiki, kwa wale wagonjwa poleni sana.

Leo nimeamua kuja na mada hii kwa sababu nimepata malalamiko kutoka kwa msomaji wangu aliyeamua kunywa sumu baada ya kuona mume wake ameoa bila kumwambia na kusubiri kuambiwa na jirani yake aliyempelekea umbeya.

Hivi wanaume mnadhani ni sahihi kuoa bila kuwaandaa wake zenu? Je, dini inasemaje katika suala hili, hakika kama wewe ni muumini wa dini inayoruhusu wanawake wanne bila shaka utakuwa unajua sheria ingawa huko sitaki kuingia zaidi ila naomba niwakumbushe wanaume mliposahau.

Simaanishi nataka muongeze wanawake kisa eti dini inaruhusu ni kwa sababu limekuwa suala la kawaida.Wanaume nawakumbusha kuwa mke ni lazima apewe haki yake ya kuelezwa na aridhie kisha ndiyo uoe, pia kuna zawadi unatakiwa kumpatia mkeo ili iwe ushahidi wa kumbukumbu.

Zawadi hiyo inaitwa ‘muago’ hiyo ni ile zawadi ambayo haiharibiki kamwe unatakiwa kumpa mkeo wakati unakwenda kuoa pale ambapo mmesharidhiana.

Kwenu nyie wanawake
Wanaume wengi wanashindwa kuwaeleza ukweli kuwa wanaoa kwa sababu ukishaambiwa tu unakimbilia kwa mganga kuzuia ndoa isifungwe.
Hivi hamjui kuwa mwanamke kukubali ukewenza anapata thawabu kubwa au hilo hamkufundishwa mlipokuwa mkiingia kwenye ndoa?

Niwakumbushe tu mume hata ukimkatalia kuoa kama ana lengo tayari ataoa tu huenda akafanya siri na wewe usitambue sasa nakusihi mwanamke mwenzangu kama mume atakwambia anaoa wewe jifunge mkanda ujue jinsi ya kulikabili.

Wanawake wengine, mume akishaoa basi yeye ndiyo anachuja kwa maumivu, nakusihi usiumie kabisa wewe jipende na ikibidi ndiyo uongeze manjonjo na ujipambe zaidi, kama kuna kitu amefuata kule asije kukuacha kabisa.

Wanaume mnaooa kwa siri
Kumbuka kuwa mume anauma sana, nawasihi wanaume mnaofanya hivi muache kwani mwanamke akisikia mume wake ameoa hawezi kuvumilia anaumia sana kama umeshaayavulia nguo maji yaoge kabisa.

Tukutane siku nyingine kwa mada kali zaidi, niwatakie mwaka mpya mwema.

Leave A Reply