The House of Favourite Newspapers

Kura ya maoni marekebisho ya katiba Rwanda yaanza

0

rwanda (1)Raia wa Rwanda akipiga kura ya maoni.rwanda (2) Wananchi wakiwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kupiga kura iwadie.rwanda (3) …wakisikiliza moja ya midahalo nchini humo.rwanda (4) …wadau wa sheria wakiwa katika moja ya midahalo kujadili urekebishwaji wa katiba ili kumruhusu rais Kagame kugombea urais kwa muhula wa tatu.rwanda (5) Rais wa Rwanda, Paul Kagame.rwanda (6)…kwenye chumba cha kupigia kura.

Raia wa Rwanda leo wanashiriki kupiga kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi na mapema, huku watu milioni 6 wakitarajiwa kupiga kura.

Rais Kagame anatarajiwa kupiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali. Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Kagame kusalia madarakani hadi 2034.

Marekani imetoa wito kwa Rais Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017. Lakini kiongozi huyo ameyashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.

Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa.

Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa rais kutoka miaka saba hadi miaka mitano, na kudumisha muda wa mihula miwili, sheria hiyo haitaanza kutekelezwa hadi mwaka 2024.
Hii ina maana Bw Kagame atakuwa huru kuwania urais kwa mihula mingine miwili ya miaka mitano mitano.

Leave A Reply