The House of Favourite Newspapers

Kutana na Mrembo Anayeishi Makaburini na Mpenzi Wake

0

MREMBO Mghana kwa jina Abena amesimulia namna alifaulu kuishi miongoni mwa wafu katika Makaburi ya Osu jijini Accra, Ghana.

 

 

Katika mahojiano na EyeGhana ambayo tumeiona kwenye ukurasa wao rasmi wa YouTube, Abena alisema huwa ana uoga sana lakini hana budi ila kuvumilia hali ilivyo.

 

 

Kulingana naye, alifanya uamuzi huo wa kuishi makaburini na mpenzi wake kwa sababu ya kushindwa kulipia makazi bora.

 

 

Abena, ambaye anaoneokana kuwa na miaka 20, alisema mara ya kwanza kuishi na mpenzi wake makaburini, alikuwa anahofia kuwa huenda baadhi ya wafu watafufuka kutoka makaburini.

 

 

Lakini mpenzi wake alimtia moyo kuwa jasiri na sasa akiwa na matumaini kuwa siku moja watahama na kuishi na watu wengine.

 

 

“Lakini mpenzi wangu aliniambia nitakapokufa, pia mimi nitakuwa miongoni mwao kwa hivyo nisiogope kwa sababu hawapo tena na hawawezi kurudi,” alisema Abena.

 

 

Leave A Reply