The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Chadema Yapata Pigo, Ntagazwa Afariki Dunia

0

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dennis Arcado Ntagazwa, amefariki dunia asubuhi ya leo, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

 

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, imeeleza kuwa taarifa zaidi kuhusu msiba wa Ntagazwa aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali tangu awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, zitatolewa hapo baadaye.

 

Mpaka anafikwa na umauti, Ntagazwa alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema.

 

 

 

Leave A Reply