The House of Favourite Newspapers

Kutimuliwa nchini Kenya, Koffi amevuna alichopanda

0

KOFFI (1)Koffi Olomide akimpiga mnenguaji wake.

Na Andrew Carlos

AMEVUNA alichopanda! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya wikiendi iliyopita ndani ya Kenya kutawala kwa sakata jingine la mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide la kumshambulia dansa wake wa kike aliyejulikana kama Pamela.

Koffi_olomide_Abracadabra_album_20111200.jpgKoffi Olomide.

Koffi a.k.a Le Grand Mopao amekuwa na matukio yanayomuweka hatiani na hili alilolifanya la kutimuliwa nchini Kenya limedhihirisha kuwa amevuna alichopanda.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2012, staa huyo aliwekwa jela miezi mitatu nchini mwao kwa kosa la kumshambulia prodyuza wake, Diego Lubaki baada ya kuombwa kulipwa pesa ya kutengeneza video.

Pia mwaka huohuo akiwa Paris, Ufaransa Koffi alifunguliwa mashtaka na madansa wake watatu baada ya kudaiwa kuwabaka na kuwafungukia ndani kinyume cha sheria.

KOFFI (2)La Kenya ilikuwaje?

Koffi alialikwa kufanya shoo siku ya Jumamosi (wikiendi iliyopita) nchini Kenya katika Ukumbi wa Bomas na ilipofika Ijumaa alikuwa amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Akiwa ameambatana na madansa wake wa kike kama ilivyo ada ya waandishi, alifanyiwa mahojiano na moja ya TV nchini humo (Citizen) na akiwa katikati ya mahojiano hayo alisikia ugomvi nyuma yake baina ya madansa wake ndipo alipoachana na mahojiano na kumvamia mmoja wa madansa wake (Pamela) na kumpiga mateke hadi pale alipoamuliwa na maafisa wa polisi wa uwanja huo.

koffiWakenya wacharuka

Baada ya kipande cha video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha udhalilishaji huo. Wakenya kwa ujumla waliungana na kukemea kitendo cha staa huyo anayebamba na Wimbo wa Selfie kuwa atimuliwe nchini humo, hafai na ameonesha kuwadhalilisha wanawake. Wakenya hao waliungana kwa kukataa msanii huyo kufanya shoo nchini humo na akamatwe mara moja kwa kuweka Hash Tag (KickKoffiOlomideBackToCongo) kwenye mtandao wa Twitter.

Ajitetea

Koffi alijitetea kuwa hakukusudia kumsha-mbulia Pamela na kwamba kwanza aliona kama dansa huyo alitaka kuibiwa pochi hivyo alienda kuamulia. Pili anasema alikuwa anajaribu kumtetea kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua madansa wake.

Atimuliwa

Baada ya taarifa kusambaa, mkuu wa polisi nchini, Kenya Joseph Boinnet alitoa taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua ambapo Ijumaa usiku alifukuzwa kwa kusafirishwa na Shirika la Ndege la Kenya Airways kwenda kwao, Kinshasa.

Wakenya wameonesha mfano

Wakenya wameonesha mfano wa kuigwa hata nchini kwetu kwa kuungana pamoja na kukemea unyanyasaji wa wanawake. Wameonesha kuwa ukatili kwa wanawake hautakiwi katika jamii na siyo kwa wanawake wa nchi yao bali kote duniani kwani dansa aliyepigwa na Koffi hakuwa Mkenya bali ni Mkongo.

Taarifa zasambaa kuwa amefutiwa maonesho Zambia

Baada ya kufanya tukio hilo la kidharirishaji la kumpiga dansa wake aitwaye Pamela, mwanamuzki Koffi Olomide taaifa zimegaa mitandaoni kuwa amefutiwa maonyesho aliyotarajia kufanya nchini Zambia.

Vyanzo vingi vya habari vimneeneza kuwa, Taasisi ya Kilimo na Biashara ya Zambia imefuta maonyesho ya mwanamuziki huyo kutoka DR Congo ambayo yalipangwa kuanza kesho Jumanne na kuendelea hadi Jumatatu ijayo.

Inasemekana Rais wa taasisi hiyo, Ben Shoko katika taarifa yake alisema kwamba kitendo alichofanya Koffi si cha kiungwana.

Ijumaa iliyopita akiwa Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, (JKIA) Nairobi, Koffi alinaswa katika video akimpiga teke dansa huyo kwa kilichodaiwa kwamba dansa huyo alikorofishana na mwanamuziki wa kundi hilo aitwaye, Cindy Le Couer ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Koffi tangu mwaka 2012.

Pamoja na kamera kumnasa, Koffi alikana kumpiga dansa huyo badala yake alijitetea kwamba alikuwa akimkinga na vibaka.

Tukio hilo mbali na kuamsha hisia za chuki kwa Koffi pia limemfanya ashutumiwe kwao DR Congo kutokana na matukio mbalimbali ya kikorofi ambayo amekuwa akihusishwa nayo.

Zambia yakanusha kufutashoo za Koffi

Kwa mujibu wa mtandao wa Lusakatimes umeripoti kuwa Taasisi ya Kilimo na Biashara ya Zambia bado inaendelea na maandalizi ya show hiyo.

“Tungependa kuwajulisha wananchi kwa ujumla kuwa mipango maonyesho ya muziki na mfalme wa rhumba Koffi Olomide yaliyopangwa kufanyika tarehe 29, 31 Julai na Agosti 1 bado lipo pale pale. Taarifa ambazo zimezagaa katika vyombo vya habari kwamba Koffi amezuiwa na onyesho limefutwa sio kweli,” taarifa hiyo imesema.

Taarifa iliendelea “Tumesha saini mkataba na Koffi wa kuja na kufanya show katika ukumbi wa Mulungushi International Conference Centre tarehe 29 Julai na zitafuata show za tarehe 31 Julai na 1 Agosti.”

Ameleta hasara kubwa

Kwa alichokifanya Koffi, kwanza ameingiza hasara kubwa kwa promota aliyeandaa shoo hiyo, pia amepoteza muda na kiasi kikubwa cha pesa kuanzia gharama ya hoteli, ukumbi, usafiri na vingine vingi.

TAZAMA KOFFI ALIVYOMPIGA DANSA WAKE NA KUKANA KUTENDA KOSA HILO AKIOHJIWA NA TELEVISHENI YA THE CITIZEN

Leave A Reply