The House of Favourite Newspapers

KUTOKA BUKOBA: MAANDALIZI YA KUMPOKEA RUGE YAMEKAMILIKA

Kaburi likingoja kumsitiri Shujaa.

BAADA wakazi wa Dar na viunga vyake kuupokea na kuuaga mwili wa mpambanaji, ‘Shujaa Muongoza Njia’ marehemu Ruge Mutahaba, mwili huo utasafiriahwa kwenda nyumbani kwao Kiziru, Kabale – Bukoba kwa ajili ya maziko.

Sheikh wa Mkoa Kagera (BAKWATA) Haruna Kichwabuta alievaa Koti, pamoja na Sheikh wa Mkoa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri, Alhaji Kamugunda wakiwa nyumbani kwa Profesa Mutahaba, Kiziru Kabale.

Hali ni shwari na nyonyo za waombolezaji zikiwa zimeajaa huzuni, simanzi na masikitiko kwa kuondokewa na kipenzi chao Ruge.

Sheikh Haruna Kichwabuta akiwa na Mzee Revelian Rwabyo mmoja wa waasisi wa wanamilia ya Mzee Mutahaba, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao marehemu Ruge kutoa pole.

Kamati ya Maandalizi chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imezidi kujipanga kwa ajili ya kuupokea ugeni Mkubwa uliombeba mpendwa wao.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akijadiliana jambo na Katibu wake, Salala Katika viwanja vya Gymkhana wakati Kamati hiyo ilipofika viwanjani hapo kuendelea kuratibu shughuli ya kuupokea ugeni wa msibani wa Ruge.

Global Publishers imezungumza baadhi ya wakazi waaeneo hayo ambao weeleza kuwa kiu kubwa zaidi kwa ndugu jamaa na marafiki kutaka kushuhudia kwani wengi hawajaamini kile wanachokiona na kukisikia Dar es Salaam na kuona kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Marekebisho yanaoendelea katika barabara ya kuelekea kijijini Kiziru Kabale – Bukoba, katika kusawazisha mashimo na baadhi ya maeneo korofi ili ipitike kiurahisi.

Kufuatia msiba huo mkubwa kwa Taifa, tayari Sheikh wa Mkoa Kagera, Alhaj Haruna Kichwabuta amefika msibani kutoa pole kwa wafiwa, mara baada ya kurejea akitokea Zanzibar akiwa akiambatana na Sheikh wa Mkoa wa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri Alhaji Kamugunda.

Kutokana na shughuli za siku ya Jumatatu (siku ya mazishi) kuhamishiwa Viwanja vya Gymkhana Kamati ipo katika mipango ya kuratibu eneo kwa ajili ya mpangilio wa majukwaa, maegesho na huduma nyingine.

Pi katika kuheshimu ukubwa wa msiba huu tayari barabara ya kuelekea Kijijini Kiziru Kabale, nyumbani kwao Marehemu imeanza kukarabatiwa ili kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa upande wa usafirishaji wa watu watakaokwenda msibani.

Viwanja vya Gymkhana ambapo shughuli nzima ya Ibada na Kuaga mwili wa Ruge itakapofanyika, kama unavyoona Kamati chini ya Mkuu wa Mkoa Kagera tayari imefika kuendelea kuratibu tukio.

Hali ilivyo sasa nyumbani tayari kaburi limekamilika likingoja kwa heshima mwili wa Ruge.

Lakini upande mwingine maandalizi yanaendelea baada ya kufungwa Turubai (tents) waombolezaji sasa wanaendelea kufika hapa kwa ajili ya kutoa pole.

Na Abdullatif Yunus |  Global Publishers, Bukoba

Comments are closed.