The House of Favourite Newspapers

Kwa nini Iringa Imekuwa Kimbilio la Waathirika wa Madawa ya Kulevya?

0

 

chid-benz

Chiddy Benz

Watu wanaathirika kwa madawa ya kulevya, wengine wanakufa wakiwa  vijana wadogo ambao walikuwa na ndoto nyingi maishani mwao ila mwisho wa siku wanakufa pasipo kutimiza ndoto zao. Mbali na watu wakawaida wanaoathiriwa na madawa hayo, pia wapo mastaa ambao kila siku wamekuwa watumiaji wakubwa wa madawa haya ya kulevya..

Tukianza na msanii wa zamani wa kundila Daz Nundaz na staa wa Wimbo wa Namba 8,Daz Baba ameone kana kwa muda mrefu mkoani Iringa akiwa nikamamtu aliyechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu

dark-master1

Dark Master.

Hali kadhalika kwa mkali mwingine aliyewahi kuchukua Tuzo ya Msanii Bora wa Rap, Chid Benz, inasemekana kwa sasa hayupo jijini Dar es Salaam na taarifa zinasema kwamba amekimbizwa mkoani Iringa na prodyuza Lamar.

Kama hiyo haitoshi, pia mwanamuziki wa Kundi la Chamber Squad, Dark Master naye kwa sasa yupo mkoani Iringa na inaelezwa kuwa hali yake kiafya ni mbaya sana. Ameathirika na dawa hizo na anatumia pombe kali kiasi cha kuhatarisha maisha yake.

Kwa nini mkoani Iringa?

iringa-sober-house

Baadhi ya vijana waliathirika na Madawa ya Kulevya wakiwa katika kituo cha kuwarudisha ‘SOBER HOUSE’ Iringa.

Taarifa za awali zinasema kwamba wasanii wengi wamekuwa wakikimbilia mkoani huko kwa sababu mbali na kituo cha kuwarudisha waathirika wa madawa hayo (Sober House) kujengwa Bagamoyo, pia kingine kimejengwa mkoani humo hali inayowafanya wengi kwenda kupata matibabu.

Ila sasa wengine wamefunguka na mtandao huu kwa kusema kuwa si wote wanaokwenda huko wanakwenda kwenye kituo hicho bali wengine huenda huko kwa kuwa wanapata madawa hayo kirahisi kutokana na uuzaji mkubwa wa siri unaoendelea huko, taarifa ambazo bado hazijathibitishwa.

 

Salum Milongo/GPL

 

 

Leave A Reply