The House of Favourite Newspapers

Kwa Nini Wanawake Wanaongoza Kwa Kupata U.T.I?

 

U.T.I ni kifupi cha (Urinary Tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri zaidi njia ya mkojo. Wanawake ndiyo wanaongoza kwa kuupata ugonjwa huu kwa urahisi sana kuliko wanaume kwa vile mirija ya mkojo ya mwanamke ni mifupi ambayo huruhusu bakteria kupita kwa urahisi tofauti na mwanaume.

Katika magonjwa yanayosumbua wanawake wengi na watoto nchini hivi sasa ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo. Wakati wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu wakihangaika kila kukicha kupata tiba yenye usahihi, wataalamu wa afya wanasema unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo.

Tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo unaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema, huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya sana.

Bakteria hawa hupatikana ndani ya sehemu za siri za mwanamke, bakteria hao wakiwa ndani ya uke hawana madhara kabisa, lakini pindi uke unapopata mchubuko bakteria hawa huanza kuathiri kibofu cha mkojo na mtu kuanza kupata madhara.

Wanawake wanapata U.T.I kwa urahisi sana kuliko wanaume kwa sababu mirija ya mkojo ya mwanamke ni mifupi ambayo huruhusu bakteria kuingia kwa urahisi tofauti na ya mwanaume.

Vyanzo vya U.T.I

Kuna vyanzo vingi vinavyosababisha ugonjwa huu, ikiwamo matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga huweza kuweka bakteria kwa urahisi na mwanamke kupata U.T.I.

Uchafu wa vyoo nayo huwa sababu nyingine, kwani matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha mwanamke kupata U.T.I kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha U.T.I.

Kufanya ngono mara kwa mara ni tatizo kubwa ambalo ndilo linafanya wanawake wengi kupata U.T.I siku hizi, kwani wakati wa ngono msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bakteria kutoka kupitia majimaji ya ukeni na kuingia katika njia ya mkojo.

Mwanamke ambaye anafanya ngono mara kwa mara yuko kwenye hatari ya kupata U.T.I kuliko yule ambaye hafanyi ngono mara kwa mara. Pia matumizi ya nguo za ndani za mitumba bila kufua husababisha kwa urahisi mwanamke kupata U.T.I.

Hata hivyo anasema tatizo kubwa limetajwa kuwa kemikali, kemikali zinawaathiri wanawake wengi siku hizi kutumia sana kemikali hasa kwenye vipodozi ambavyo kemikali hizi kwa kuwa ni sumu huenda hadi kwenye kibofu na kuchubua kibofu na hapo ndipo tatizo hilo huanza.

Save

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Comments are closed.