The House of Favourite Newspapers

Kwa sifa hizi, kwa mumeo utadumu!-2

0

vegeterians-couple-bedWiki iliyopita nilianza kuzungumzia sifa zinazoweza kumfanya mwanamke kudumu kwa mumewe. Leo nitazimalizia, zisome.

  1. Kulelewa

Siyo kila mwanaume anataka mtu atakayempa matunzo kama anayoweza kupata kwa mama yake. Lakini ni kwamba mwanaume anataka kujisikia anapendwa, anatunzwa kwa kiwango fulani na mwenza wake kwani wakati mwingine wanaume huwa kama watoto.

  1. Anayejitegemea

Hata kama mwanaume anapenda kupata attention kubwa kutoka kwa mpenzi wake, huwa hapendi  kumuona akimganda kama kupe, pamoja na yote muache awe peke yake wakati mwingine, afanye kile anachojisikia pia, ukimganda sana mapenzi yanapotea.

  1. Akili

Wanaume wengi wanapenda wanawake wenye akili, wenye uwezo wa kuongea na kujiamini katika mazingira yote,  kijamii, familia na mengine.

  1. Awe na Mvuto

Wanaume wengi wanapenda mwanamke mwenye mvuto, kuanzia mavazi, usafi mpaka muonekano wake, si lazima awe mrembo lakini anayevutia, bila shaka mnanielewa nikisema anayevutia.

  1. Mtu wa familia

Wanaume wanapenda wanawake wanaoweza kuilinda familia, yaani nikimaanisha kuwa mwanamke ambaye anao muda wa kuwa na familia yake ipasavyo, kuna wanawake ambao huwa hawana muda wa kukaa nyumbani na familia zao, muda mwingi huwa viwanjani kujiachia.

  1. Ushirikiano

Wanaume hupendelea kumuona mwanamke mwenye ushirikiano na wenzake ambaye atakuwa tayari kushirikiana na familia za pande zote mbili kwa ajili ya kuweka uhusiano vizuri.

Leave A Reply