The House of Favourite Newspapers

Kama Dakika Moja Inabadili Maisha, Siku 29 Je?

0

Nyumba (9) Na Ojuku Abraham, Risasi Mchanganyiko

ZIMEBAKI siku 29 tu kabla historia haijaandikwa. Siku hiyo ndiyo ambayo itashuhudia droo kubwa kuwahi kutokea, ikichezeshwa na mojawapo ya vitu ambavyo havikuwahi kabisa kufikiriwa, vitatokea.

Kutakuwa na zawadi nyingi ndogondogo zitakazotolewa, huku mamilioni ya Watanzania wakitaka kusikia kama ni kweli mtu atashinda nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 60, ambayo ipo Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Nyumba (8)Nimezungumza mara nyingi juu ya uhakika wa suala hili kutokea, kwa sababu historia ya Global Publishers inaonesha imeshafanya vitu vikubwa mara nyingi, kiasi cha kuaminika mbele ya wasomaji wa magazeti yake ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Amani na Risasi.

Ninachotaka kusema leo ni kwamba kama ulikuwa bado hujaanza kushiriki mchezo huu, bado hujachelewa kabisa. Nyumba hii ya kisasa, inaweza kuwa mali yako bila kujali upo sehemu ipi Tanzania.

Kama maisha yanaweza kubadilika ndani ya dakika moja tu, basi kuna uwezekano mkubwa wa tukio hili kubwa likabadili maisha yako ndani ya siku 29 zilizobaki, endapo tu utajitoa muhanga kuhakikisha hupitwi na magazeti haya yanapotoka, ukinunua, unafunua ukurasa wa pili, unajaza kuponi na kuipeleka kwa wakala yeyote wa Global Publishers popote ulipo nchini.

Kuna watu wanadhani kwa kuwa zoezi hili limeanza miezi sita iliyopita, basi kama walikuwa bado hawajaanza kushiriki, hawana nafasi ya kushinda. Kama una mawazo haya, nataka nikukumbushe kuwa anayepanga riziki ni Mungu.

Unaweza kuwa hujawahi kucheza, lakini ukanunua kuponi moja tu na ukaibuka mshindi kwa sababu kuponi zote lazima zitatumbukizwa kwenye pipa.

Kwa ajili hiyo, usijali, bado hujachelewa kuitwaa nyumba hii ya kisasa kwa shilingi mia tano tu, ambayo ni bei ya magazeti hayo.

Wapo baadhi ya watu wanakatisha wenzao tamaa kwa kuwaambia kuwa Global Publishers haiwezi kutoa nyumba. Niwathibitishie kwamba tukio hili ni la kweli na litatokea Juni 30, mwaka huu wakati wa uchezeshaji wa droo kubwa.

Kampuni hii pia imewahi kutoa zawadi kubwa za magari kama Mercedes Benz, Toyota Prado, Toyota Noah, Toyota Vitz na Fun Cargo, achilia mbali zawadi kama pikipiki za kila aina, vyombo vya nyumbani, simu za kisasa, seti za televisheni za kisasa na vitu vingine kedekede.

Unaweza kudharau leo, halafu siku ikifika, unashangaa mtu unayemfahamu, ndiye anakabidhiwa hati ya nyumba hiyo, kitu ambacho hata wewe unaweza.

Umepoteza fedha ngapi kwa mambo ambayo hayakuwa hata na uwezekano wa kukupatia faida. Hebu shiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba uibuke mshindi na kumiliki nyumba hiyo ya kisasa yenye samani ndani.

Leave A Reply