The House of Favourite Newspapers

Kwa sifa hizi, kwa mumeo utadumu!

0

blackcouple-bedsmileMapenzi kama yanavyosemwa na watu ni sanaa kama sanaa zingine zilivyo. Kama ni mchezo, basi una sheria zake. Leo shoga yenu Shangingi Mstaafu nakupa vigezo muhimu ambavyo, ukivizingatia, mumeo hakuachi hata kwa dawa!

  1. Upendo

Kila mwanaume anataka kujisikia anapendwa. Anataka kuona kuwa mwenza wake anampenda kiuhalisia na anamjali.

  1. Heshima

Hata pale anapokuwa hayupo, anataka mwenzake wake awe nyuma yake, kumuongelea na kumheshimu.

  1. Mahaba

Kila mwanaume anahitaji mahaba, hapa nasema mahaba badala ya ngono, kwa sababu si kila mwanaume ni mzuri katika hilo. Mahaba ninayoyaongelea ni kupapaswa, kubusiwa au kukumbatiwa.

  1. Kukubalika

Kila mwanaume anataka kujisikia mwenza wake anamkubali na kumthamini kwa mambo mbalimbali kama vile penzi lake, muda, jitihada, anavyojituma na kila anachokifanya kwa mwenza wake.

  1. Yeye ni bora zaidi

Anataka mwenza wake kujisikia kuwa yeye ni bora zaidi. Kila mwanaume anataka ajisikie kuwa yeye ni mwanaume bora zaidi kuliko wote aliowahi kuwa nao, na wengine wanataka kujisikia kuwa ni mwanaume pekee ambaye umewahi kuwa naye hata kama anajua si kweli.

  1. Uaminifu

Mwanaume anahitaji mwenza wake awe mwaminifu. Uaminifu husaidia kujenga mapenzi zaidi, kila kitu kwa mwanaume na kadiri mwenzake anavyokuwa mwaminifu, ndivyo hawezi kuwa na wivu kwani anakuwa ameshajiaminisha.

  1. Ukweli

Kila mwanaume anahitaji kujua kuwa anaweza kumwamini mwenza wake na kwamba naye anamwamini, ukiwa mkweli ni rahisi mume kukujengea imani, kuwa mkweli kwa kila jambo.

Itaendelea wiki ijayo.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply