The House of Favourite Newspapers

LAAC yaagiza ukamilishaji ujenzi wa shule mpya Kigera Mwiyale, Musoma

0

KAMATI ya kudumu ya Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kuhakikisha inakamilisha kwa wakati Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kigera Mwiyale ili kuanza kutoa huduma kwa jamii

Kauli hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Staslaus Mabula (Mb) Machi 24,2024 wakati kamati ikikagua ujenzi wa shule hiyo pamoja na kituo cha afya cha Rwamlimi,Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara.

Mabula amesema licha ya Halmashauri kuomba nyongeza ya fedha kiasi cha shilingi milioni 153 kwa ajili ya kamilishaji wa ujenzi huo,Kamati inaagiza ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

“Inashangaza kuona Halmashauri nyingi zimekamilisha ujenzi wa shule hizo za kata lakini hapa majengo mengi hayajakamilika kama vile maktaba,maabara,jengo la utawala na jengo la TEHAMA,niwatake majengo haya yakamilike na yaanze kutumiwa na wanafunzi”amesisitiza Mabula.

Kamati imeelekeza ujenzi wa shule ukamilike kwa wakati na nyongeza za fedha ziendane na uhalisia wa ongezeko la gharama kusudiwa.

“Sio kama tumesema shule ikamilike kwa wakati ndio iwe chanzo cha ongezeko la gharama bali gharama za nyongeza zizingatie uhalisia “amesisitiza Mabula

Kwa upande wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Rwamlimi Kamati imepongeza halmashauri kwa ukamilishaji wa majengo hayo kwa wakati hivyo wameishauri kutumia mapato ya ndani kujenga njia za watembea kwa miguu ili kuwa na hadhi inayostahili.

Naye Meya wa Manispaa ya Musoma Mheshimiwa William Gumbo ameishukuru Kamati hiyo na kuahidi kusimamia kikamilifu miradi yote inayotekelezwa na Halmashauri hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Stori na Angela Msimbira MUSOMA

MSIMU MPYA MAMBO MAPYA!
Gazeti lako bora la Championi linalotoka mtaani mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa, sasa limekuja kivingine.
Tunatoa zawadi kwako ewe msomaji ambapo kwa kununua GAZETI LA CHAMPIONI, utapata fursa ya kuzawadiwa jezi mpya ya Simba au Yanga za msimu wa 2023/2024, pindi ununuapo gazeti letu kupitia Global App.
Soma Gazeti la Championi kwa urahisi mtandaoni kupitia Global App: https://globalapp.co.tz
Leave A Reply