The House of Favourite Newspapers

Matinyi: Waziri Ndumbaro Alikuwa Anatania Suala La Ukaguzi Wa ‘Passport’

0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema “Lugha za michezo utani ni kitu cha kawaida, mnapozungumza 80% ni utani na 20 ndio ukweli, mkizungumza habari za #Simba na #Yanga ukang’ang’ana kitu kama kilivyoandikwa utafika hatua utawachosha Watu.”

Matinyi amesema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro aliyedai ukaguzi utafanyika Uwanja wa Mkapa kwa mashabiki watakaovaa jezi za timu za wapinzani wakati wa michezo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Yanga na Simba ni washiriki

Amesema “Si kweli kuwa Waziri alimaanisha kutakuwa na ukaguzi wa Passport, anayehusika na ukaguzi ni Idara ya Uhamiaji ambayo hakuitaja alipozungumza, Watu wamekomaa na utani hadi Mamelodi wamesikia, wameingia uoga hadi TFF wameamua kuandika barua kuwaeleza suala hilo halipo.”

#PART 1: MWANAFUNZI ADAI KUBAKWA – APATA UJAUZITO NA KUACHA SHULE – ALIPATA DIVISION 2…

Leave A Reply