Lava Lava Amkataa Uwoya

ANA shepu bufalo, mwendo kama hakanyagi chini (hakanyagi chini), njonjo kangaroo, kafungasha double kibini (double kibini), ana guu la bia tende, kifuani dodo embe, kipotabo Dayna Nyange, akitembea ndembe ndembe, yani kama mzembe, mambo yote pambe…” Hii ni sehemu ya mashairi ya Ngoma ya Niuwe.

 

Ukiisikia ngoma hii ambayo haikosekani kwenye laptop za ma-DJ wa klabu za starehe, lazima utauliza ni wa msanii gani?

Usipate taabu! Ni ngoma ya dogo mmoja wa pale Wasafi Classic Baby (WCB), Mr Love Bite, wengi wanamjua kama Lava Lava.

 

Jina kamili ni Abdul Iddi.

Mbali na Niuwe, Lava Lava anasikika vizuri kwenye midundo ya ngoma zake kali kama Go Gaga, Bora Tuachane, Kilio, Gundu, Utatulia, Tekenya na nyingine kibao ambazo zimetazamwa na mamilioni kwenye YouTube.

Lava Lava ana mengi ambayo ameonesha kwenye muziki wake, lakini kuna yale ambayo watu hawayajui.

 

IJUMAA SHOWBIZ imekaa kitako na Lava Lava, ambapo anafunguka mambo kibwena kuhusu muziki wake na uhusiano wake na staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ambapo kumekuwa na tetesi kuwa anatoka naye kimapenzi;

 

IJUMAA SHOWBIZ: Mashabiki wameshakusikia kwenye ngoma kadhaa. Je, kwa sasa nini mipango yako?

LAVA LAVA: Mipango iko mingi. Kwa sasa tunafanya Usiku wa Kwio na vitu vingine vingi ambavyo siwezi kuvisema kabla havijakamilika, hivyo watu watajua tu.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Wasanii wengi wamekuwa na utaratibu wa kuachia EP (Extended Play) au albam, kwa upande wako hizo ishu zimekaaje?

LAVA LAVA: Utaratibu huo ni mzuri na mimi kwa upande wangu ninajipanga kuachia EP au albam, lakini kwa upande wa uongozi (Wasafi) bado kuna vitu wanaweka sawa, vikishakuwa tayari, mashabiki watajua tu.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Wasanii wa WCB mnaonekana kugeukia muziki wa Singeli, je mnadhani huko ndiko kwenye soko zaidi?

LAVA LAVA: Naweza kuzungumzia kwa upande wangu, watu wajue kwamba Singeli ni aina ya muziki ambao unaelezea maisha halisi ya Kitanzania. Hivyo, hata Meja Kunta alipokuja kuniomba kolabo ya Ngoma ya Wanga, niliona ni sawa, japokuwa kwa mara ya kwanza nilimkatalia, lakini baadaye nikaona mimi ni mtoto wa Kiislam, siyo vizuri ukiombwa kitu ukatae. Nikaona acha nimsaidie kwa sababu alikuwa ametoka kwenye matatizo (alidaiwa amekufa).

 

IJUMAA SHOWBIZ: Unaizungumziaje Ngoma ya Wanga ambayo imekuwa gumzo hadi Marekani?

LAVA LAVA: Kwanza niseme kuwa Meja Kunta ni kijana ambaye anajituma sana ndiyo maana nikaamua kufanya naye kazi na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu, Wanga ni ngoma ambayo imefanya vizuri na bado inaendelea kutikisa. Kikubwa zaidi ni kukubalika na msanii mkubwa wa Marekani (Swizz Beatz).

 

IJUMAA SHOWBIZ: Una mpango wa kuendelea kuimba Singeli?

LAVA LAVA: Kwa sasa hivi hapana, ila kama itatokea nitafanya.

IJUMAA SHOWBIZ: Kiba si mtu wa kusifia sana, lakini ameisifia ngoma yako ya Bora Tuachane, kwa upande wako unalichu-kuliaje?

 

LAVA LAVA: Ni kweli na ninaelewa kuwa Ali (Kiba) si mtu wa kusifia sana ngoma za wasanii wengine, lakini kwa yeye kuisifia Bora Tuac-hane, kwa upande wangu, nilijisikia faraja kubwa kwa sababu ni mtu amb-aye anata-mbua vipaji vya watu, hivyo nin-ams-huk-uru.

IJUMAA SHOWBIZ: Je, umepanga kufanya naye kolabo?

 

LAVA LAVA: Ndiyo naweza kufanya naye, ila kama pande zote mbili zitakubaliana kwa sababu yeye ana menejimenti yake na mimi nina menejimenti yangu.

IJUMAA SHOWBIZ: Umeshawahi kuwaza kujitoa WCB na kujisimamia mwenyewe?

LAVA LAVA: Hapana, sijawahi kuwaza kutoka WCB na sioni sababu ya mimi kutoka wasafi.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Muziki wa sasa umekuwa na ushindani hasa kwa wasanii kutoka WCB. Je, wewe unaitunza vipi ‘status’ yako usishuke kwenye soko?

LAVA LAVA: Nakubali kabisa kwamba muziki wa sasa una ushindani na hakuna kitu kisichokuwa na ushindani, ila kikubwa ni mimi mwenyewe kuilinda hadhi na jina langu, maana kila msanii anapokelewa na mashabiki kutokana na vile anavyojiweka. Kingine ni kufanya kazi kwa jitihada. Pia kutoa ngoma nyingi, ni hivyo tu.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Kuna tetesi kuwa upo kwenye penzi zito na Uwoya. Je, tutegemee ndoa?

LAVA LAVA: Hakuna siku ambayo tulitangaza kuwa tuna uhusiano, watu wanatengeneza maneno tu na kuyasambaza, mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Irene (Uwoya).

IJUMAA SHOWBIZ: Lakini mnaonekana mkiwa pamoja sehemu nyingi.

 

LAVA LAVA: Hapana, Irene hajawahi kuwa mtu wangu na wala kwenda naye sehemu yoyote. Huo ni umbea tu, watu wanautengeneza na mimi ndiyo najua ukweli kuwa hakuna kinachoendelea maana nina uhusiano na mtu mwingine tofauti na huyo Irene.

IJUMAA SHOWBIZ: Inasemekana wasanii WCB hampendi ndoa na kwenu ni mtihani, unalizungumziaje hilo?

 

LAVA LAVA: Hakuna kitu kama hicho kwa sababu ndoa ni baraka na majaaliwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kama ikifikia wakati wa kuoa, mtu unaoa tu. Hata kwa upande wangu, ukifika wakati na nikapata mtu sahihi, basi naoa. Hilo ni jambo la heri.

IJUMAA SHOWBIZ: Je, mashabiki wategemee kazi ya pamoja kutoka kwako, Mbosso na Rayvanny maana hamjawahi kutengeneza ngoma ya pamoja?

 

LAVA LAVA: Hiyo ni mipango ya kiuongozi, kwa mimi siwezi kuzungumzia.

IJUMAA SHOWBIZ: Unamzungumziaje Diamond Platnumz?

LAVA LAVA: Ni mtu ambaye nikianza kumzungumzia, naweza kumaliza kurasa maana ana vitu vingi vizuri vya kumuelezea. Pili ni mtu ambaye anasaidia sana hasa vijana wenzake, anajali, anajua utu ni nini. Kiukweli ana mambo mengi mazuri.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Kwa upande wako, kolabo za kimataifa zipo au unategemea kufanya?

LAVA LAVA: Zipo, lakini utakapofika muda muafaka wa kuzungumzia hilo, basi nitazungumza maana ni exclusive.

 

Lava Lava alitarajia kuangusha shoo ya kihistoria inayokwenda kwa jina la Usiku wa Kwio katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, usiku wa Machi 21, mwaka huu, lakini kutokana na Corona, shoo hiyo imehairishwa.

MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA NA KHADIJA BAKARI

Toa comment