Muumini: Mimi Siyo Kocha wa Dunia Tena

MKONGWE wa dansi ambaye kwa sasa anasimamia Bendi ya Shadai, Mwinjuma Muumini amesema, kwa sasa hana sifa ya kuitwa Kocha wa Dunia kama wanavyomjua mashabiki wake kwa sababu amefulia.

 

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Muumini alisema, kutokana na kupotea muda mrefu na kupoteza ramani, sasa hivi amepata bendi mpya ya Shadai na kuamua kutunga kabisa kibao cha kufulia.

 

“Nilipotea muda mrefu na sina hadhi tena ya kujiita Kocha wa Dunia maana nimefulia mno tofauti na wanamuziki wengine, ndiyo maana nikaamua kuachia Wimbo wa Nimefulia kupitia bendi yangu mpya ya Shadai,” amesema Muumini ambaye aliwiki zamani akiwa kwenye bendi mbalimbali za dansi.

STORI: IMELDA MTEMA

 

Toa comment