The House of Favourite Newspapers

Lava Lava Kusepa Wasafi?

0

JUNI 29, mwaka huu, Diamond Platnumz ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Wasafi aliachia video ya wimbo wake wa Kamata baada ya kukaa kimya kwa takribani miezi saba.

 

Diamond alisema kuwa, ukimya huo ulitokana na majukumu aliyokuwa nayo ya kuandaa albam yake mpya ya nne baada ya kuachia Kamwambie (2010), Lala Salama (2012) na A Boy From Tandale (2018).

 

Hata hivyo, kwenye video hiyo ya Kamata kulikuwa na kitu kinachotajwa kama ishara f’lani.

Ni hivi; Lava Lava alionekana kwenye video hiyo; sawa na Harmonize na Rich Mavoko walivyotokea kwenye video nyingine ya Diamond ya Hallelujah iliyotoka Septemba 28, 2017 akiwashirikisha Morgan Heritage.

 

Hata hivyo, wawili hao (Harmonize na Rich Mavoko) tayari wamejitoa kwenye lebo hiyo na kwenda kuanzisha zao. Je, itakuwa hivyo kwa Lava Lava naye?

STORI; IJUMAA WIKIENDA, DAR

Leave A Reply