The House of Favourite Newspapers

Leicester City Wamtimua Kocha Wao Claudio Ranieri

LEICESTER, ENGLAND;

TAARIFA ya kusikitisha ikufikie wewe mpenda soka popote ulipo kwenye kona ya dunia. Hii ni baada ya usiku wa February 23, 2017, uongozi wa Klabu ya Leicester City ambao ni Mabingwa Ligi Kuu ya Uingereza kutangaza kuamua kumfuta kazi rasmi aliyekuwa kocha wake mkuu wa Claudio Ranieri, kufuatia kutofanya vizuri katika Ligi hiyo.

Katika Msimu huu, Leicester City imekuwa ikiyumba kutoka kutwaa taji la EPL msimu wa 2015/2016 hadi kushika nafasi za kuwania kutoshuka daraja, kwa sasa ipo nafasi ya 17 katika Ligi Kuu England na ilipoteza na timu ya Millwall kutoka League One katika mchezo wa FA Cup msimu huu.

Hata hivyo, hadi sasa Leicester City imecheza jumla ya mechi 25 katika Ligi Kuu England, ikiwa imebakiza jumla ya mechi 13, imeshinda jumla ya mechi 5, sare mechi 6 na imekubali vipigo katika mechi zake 14 msimu huu na ina point 21 ikiwa katika hatari ya kuwania kutoshuka daraja.

Comments are closed.