The House of Favourite Newspapers

LEMA ATII WITO WA POLISI, AWASILI SENTRO KUHOJIWA – VIDEO

MBUNGE wa Arusha Mjini (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema ameitikia wito wa Jeshi la Polisi na kuwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini humo leo Oktoba 22, 2018 lakini haijafahamika ameitwa kwa sababu gani.

Lema ambaye jana alipigiwa simu na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi na kumtaka afike kituoni hapo leo, amewasili akiwa ameongozana na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lema ameandika; Nimepigiwa simu na Polisi kwamba natakiwa kuripoti kituo kikuu cha Polisi Arusha leo bila kukosa,sijaelezwa sababu lakini wito unaonekana kuwa wa lazima sana,lakini nafikiri kupigania haki ndio linaweza kuwa kosa langu kubwa. MSIOGOPE.” amesema Lema.

 

BREAKING: LEMA alivyotinga Polisi leo, Ishu ya ‘Mo Dewji’

Comments are closed.