The House of Favourite Newspapers

Licha ya matatizo yake ya kiafya Penny: shisha siachi

0

26f29e9cdff937646b22556173b02244Peniel Mungilwa ‘Penny’

Na Imelda Mtema
MTANGAZAJI mwenye jina ambaye pia ni MC, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amedai licha ya matatizo yake ya kiafya, hawezi kuacha kuvuta kilevi aina ya shisha kwani harufu yake inamfanya ajisikie vizuri.

Alitoa kauli hiyo huku kukiwa na madai kuwa amekuwa akitibiwa mara kwa mara maradhi ya pumu na wakati mwingine kulazwa hospitalini, lakini anapopata nafuu huanza tena kuvuta, kitu kinachomuongezea matatizo yanayohatarisha maisha yake.

“Siwezi kupinga kuwa sivuti Sisha, lakini mimi napenda kusikia harufu yake na si kitu kingine na hata kama kuvuta siyo kihivyo kabisa na pia nitajitahidi kama naweza kuiacha maana inanichanganyaga,” alisema Penny.

Leave A Reply